Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madhila kwa wananchi wa Syria sasa yamefurutu ada: Panos Moumtzis

Mapigano Kusini Magharibi mwa Syria yanaweka hatarini maisha ya watu  wengi wakiwa ni watoto, kama hawa pichani  waliokimbia Deraa.
UNICEF/Al-Faqir
Mapigano Kusini Magharibi mwa Syria yanaweka hatarini maisha ya watu wengi wakiwa ni watoto, kama hawa pichani waliokimbia Deraa.

Madhila kwa wananchi wa Syria sasa yamefurutu ada: Panos Moumtzis

Amani na Usalama

Hali ya kibinadamu nchini Syria inazidi kudorora, machafuko yakiongezeka Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo na kusababisha wanawake, watoto na wanaumbe Zaidi ya 30,000 kutawanywa katika siku chache zilizopita nma wengine wengi wakipoteza maisha ya kujeruhiwa.

Hayo yamesemwa na mratibu wa masuala ya kibinadamu wa kikanda Panos Moumtzis akisisitiza kuwa hofu ya Umoja wa Mataifa na shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA ni kwamba huenda zahma kubwa zaidi inakuja.

Hivi sasa kuna watu milioni 6.2 ambao ni wakimbizi wa ndani nchini Syria, huku usalama na ulinzi kwa raia  milioni 2.9 wanaoshi Idlib na viunga vyake uko hatarini. Watu hao ni pamoja na wakimbizi wa ndani milioni 1.4 wengi wao wakiwa wanawake na watoto ambao waliwasili jimboni humo baada ya kukimbia machafuko sehemu zingine.

Ameongeza kuwa machafuko Zaidi yatasababisha watu wengi Zaidi kutawanywa  katika eneo ambalo tayari lina idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani. Watu hao wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo za mahitaji muhimu ya kibinadamu na kushindwa kuondoka katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika na vita na kuwaacha wakihitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR amesema ukata wa ufadhili unatishia misaada ya kibinadamu kwa mamilioni ya wakimbizi na wakimbizi wa ndani nchini humo.

Hivi sasa dola milioni 270 zinahitajika haraka ili kuhakikisha kwamba mamilioni ya wasiojiweza hususan wakimbizi na wakimbizi wa ndani hawakosi mahitaji muhimu ya msingi kwa mwaka huu ikiwemo maandamizi muhimu yanayohitajika kwa ajili ya msimu wa majira ya baridi kwa wakimbizi hao.