Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mshambuliaji wa kujilipua aua watu 19 Afghanistan, UN yatoa kauli

Baada ya shambilizi la kigaidi nchini Afghanistan
UNAMA/Jawad Jalali (file)
Baada ya shambilizi la kigaidi nchini Afghanistan

Mshambuliaji wa kujilipua aua watu 19 Afghanistan, UN yatoa kauli

Amani na Usalama

Hii leo huko jijini Jalalabad, jimbo la Nangarhar nchini Afghanistan, mshambuliaji wa kujilipua amesababisha vifo vya watu 19 na wengine 20 wamejeruhiwa.

Shambulio hilo lilitokea Jumapili wakati watu walipokuwa wamekusanyika wakisubiri kumlaki Rais Ashraf Ghani wan chi hiyo.

Umoja wa Mataifa unasema miongoni mwa wahanga wa tukio hilo ni raia na watoto kutoka jamii ya wahindu na masingasinga.

Kufuatia tukio hilo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa wafisa na serikali ya Afhganistan huku akitaka ahueni ya haraka majeruhi.

 

Kambi ya Samar Khel, karibu na Jalalabad.Raia wa Afghanistan waliotatizwa na vita ndio walikuwa wanakaa.
Bilal Sarwary/IRIN
Kambi ya Samar Khel, karibu na Jalalabad.Raia wa Afghanistan waliotatizwa na vita ndio walikuwa wanakaa.

Amesema shambulio lolote lile la makusudi dhidi ya raia halikubaliki kwa misingi yoyote ile na kwamba ni ukiukwaji wa haki za kibinadamu za kimataifa.

Katibu mkuu kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake amesihi pande zote husika nchini Afghanistan kuzingatia wajibu wao wa kulinda raia ikiwemo jamii za wachache na kusitisha kulenga raia na miundombinu yao ya kijamii.

Amesema Umoja wa Mataifa unasimama kidete na serikali ya Afghanistan wakati huu wanaposaka Amani na maridhiano kwenye nchi yao.