Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanjo ya kunusuru watoto dhidi ya kuhara yazinduliwa Uganda:UNICEF

WHO inapendekeza  kampeini ya chanjo dhidi ya virusi vinavyosababisha kuharisha
UN
WHO inapendekeza kampeini ya chanjo dhidi ya virusi vinavyosababisha kuharisha

Chanjo ya kunusuru watoto dhidi ya kuhara yazinduliwa Uganda:UNICEF

Afya

Chanjo itakayo wakinga watoto wa chini ya muri wa miaka mitano na virusi vinavyosababisha kuhara (rotavirus) imezinduliwa nchini Uganda kwa ushirikiano wa serikali na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. 

Chanjo hiyo iliyozinduliwa rasmi Jumatatu katika wilaya ya Buikwe, itatolewa bure kwenye vituo vyote vya afya nchini Uganda na inatarajiwa kuokoa maisha ya maefu ya watoto wanaofariki Dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa wa kuhara.

Mwakilishi wa UNICEF, nchini Uganda Dokta Doreen Mulenga, ameipongeza seriali ya Uganda kwa kujumisha chanjo ya rotavirus katika mpango wa chango wa kitaifa na kusema ni hatua muafaka katika juhudi za kutimiza lengo la afya bora kwa watoto wote.  

Mtoto akipewa chanjo
UNICEF/Dejongh
Mtoto akipewa chanjo

 

Dokta Mulenga ameongeza kuwa chanjo hiyo ni ya muhimu sana katika kudhibiti magonjwa mengi hatari kwa watoto, na amewahimiza wazazi na walezi wa watoto kuhakikisha watoto wao wamechanjwa.

Akionyesha matumaini kuhusu chanjo hiyo, Dokta Jane Ruth Aceng, wazri wa afya wa Uganda amesema, watoto 10,637 walio chini ya umri wa miaka mitano wanakadiriwa kupoteza maisha kila mwaka baada ya kuambukizwa virusi vya rota.Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la afya Ulimwenguni, WHO, watoto 450,000 hufariki Dunia kila mwaka duniani kote kutokana na virusi hivyo.