Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres amelaani vikali shambulio nchini Zimbabwe

Bendera ya Zimbabwe
UN Photo/Loey Felipe
Bendera ya Zimbabwe

Guterres amelaani vikali shambulio nchini Zimbabwe

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ashtushwa na kulaani mlipuko uliotokea nchini Zimbabwe Jumamosi.

 Antonio Guterres ametaka wahusika wa shambulio hilo kufikishwa mbele ya mkono wa sheria. Watu zaidi ya 40 wakimewo wana siasa wa ngazi ya juu wamejeruhiwa na wengine kupoteza maisha baada ya mlipuko kutokea wakati wa  mkutano wa kampeini za uchaguzi nchini Zimbabwe.

Mkutano huo ulikuwa ni wa chama tawala cha ZANU-PF mjini Bulawayo na mlipuko ulitokea muda  mfupi baada ya rais Emmerson Mnangagwa kumaliza hotuba yake.

Rais ambaye pia ndio kiongozi wa chama tawala, na ameripotiwa kusema kwamba shambulio hilo lilikuwa  jaribio dhidi ya maisha yake na ameomba kuwepo kwa amani na umoja wa kitaifa kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Julai 30. 

Nimeshtushwa na taarifa za mlipuko Zimbabwe

Rais huyo ameapa kuwa mlipuko huo hautazuia upigaji kura.

Rais Mnangagwa, alichukua hatamu za uongozi wa nchi hiyo Novemba mwaka jana baada ya kujiuzulu kwa rais Robert Mugabe, aliyeiongoza Zimbabwe kwa kipindi cha miaka 37.

Katika taarifa yake iliyotolewa jumapili na msemaji wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema taarifa za mlipuko huo zinasikitisha na mewatakia ahuweni ya haraka waliojeruhiwa.

 

Makamu wawili wa rais ni Miongoni mwa watu zaidi ya 40 waliojeruhiwa wakiwemo pia waandishi wa habari wa televisheni ya taifa na vilevile wanausalama.