Kumbe ndoto zangu kupinga matumizi ya plastiki sio za abunuwasi:Wakibia

8 Juni 2018

Kampeni ya kupiga vita matumizi ya plastiki ambayo sasa inashika kasi kimataifa haikuanza leo wala jana , kuna walioliona tatizo hili zamani na kulivalia njuga binafsi, miongoni mwao ni kijana kutoka Kenya kama inavyotanabaisha taarifa ya Siraj Kalyango

James Waikibia kutoka county ya Nakuru nchini Kenya  amekuwa akibeba bango la kauli mbiu ya mwaka khuu ya kupinga matumizi ya plasiki kwa miaka sita sasa.

Nahisi vizuri sana

(SAUTI YA JAMES WAKIBIA)Na kampeini yake imekuwa ikijikita katika masuala mawili,  mosi  amekuwa akikusanya taka hizoza plastiki na kisha kuzichoma na pili kuandika makala mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii kuhusu taka hizo kwa lengo kuwachagiza wananchi kuachana na matumizi ya plastiki. Leo hii siku ya baharí anahisi vipi kuona juhudi na jasho lake havikupotea bure, vimechukuliwa na Umoja wa Mataifa kupitia kauli mbiu ya mwaka huu?

Chembe chembe za plastiki zilizoko baharini zimeelezwa kuwa ni nyingi,  Wakibia  anafunguka kuhusu hatua za kuchukua kukabili changamoto hiyo.

(SAUTI YA JAMES WAKIBIA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud