Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa dunia unazidi kuimarika japo bado kuna hali ya sintofahamu :UNDESA

Dola za kimarekani
Picha ya UN
Dola za kimarekani

Uchumi wa dunia unazidi kuimarika japo bado kuna hali ya sintofahamu :UNDESA

Ukuaji wa Kiuchumi

Mchumi mkuu wa Idara ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na masuala ya kijamii UNDESA, asema matarajio ya muda mfupi kwa uchumi wa dunia yameendelea kuboreka lakini ameonya kwamba hali ya sintofahamu bado pia inaendelea.

Akiwasilisha ripoti ya awali ya uchumi wa dunia na matarajio, Katibu Mkuu msaidizi wa UNDESA Elliot Harris, alisema utabiri wa pato la dunia kwa mwaka huu na mwaka 2019 tayari umeshapitiwa kwa sababu ya  kuimarika kwa  uchumi katika nchi zilizoendelea

(Sauti ya Eliot Harris)

Viashiria muhimu katika ukuaji wa uchumi ni ongezeko la mapato na matumizi, mazingiria mazuri ya uwekezaji, pamoja na uwekezaji wa fedha kwenye mzunguuko, uliofanwya na Marekani ili kukabiliana na  athari za muda mfupi

Bwana Harris ameongeza kuwa wakati kuna habari njema kuhusu ukuaji wa Uchumi, badokuna haja kubwa yakutobweteka katika utekelezaji wa malengo ya maendelea endelevu ya mwaka 2030.

(Sauti ya Eliot Harris)

Leo hii tunakabilia na changamoto katika utekelezaji wa sera za  kimataifa za pamoja. Katika shirika kama hili uundaji wa sera za pamoja ni jambo muhimu sana , ila tofauti zetu zinaongezeka ,na  si rahisi kushughulikiwa kwa ufanisi kwa njia iliyogawanyika.