Utumiapo mara moja kijiko cha plastiki na kukitupa wajua kinapoishia?

17 Mei 2018

Baada ya kushiriki na kufanikisha mafanikio ya kampeni ya kutokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki nchini Kenya, mwanaharakati na mpiga picha nchini humo James Waikibia amesema hivi sasa ameelekeza nguvu zake kwenye kutokomeza matumizi ya vifaa vya plastiki vinavyotumika mara moja na kutupwa.

Vifaa hivyo ni pamoja na vijiko, umma, sahani na visu ambayo matumizi yake yameshamiri sana hivi sasa kila kona duniani.

Bwana Waikibia katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amesema amejikita kutokomeza matumizi ya vifaa hivyo nchini Kenya kwa kuwa..

 (Sauti ya James Waikibia)

Bwana Waikibia ambaye anaendesha kampeni yake kwa kupiga picha zinazoonyesha madhara ya utupaji hovyo taka zikiwemo plastiki amesema anafahamu vita vya kutokomeza vifaa hivyo itakuwa ni ngumu lakini ni vyema kufahamu kinachotokea kutokana na utupaji holela wa vifaa hivyo..

 (Sauti ya James Waikibia)

Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 14 la malengo ya maendeleo endelevu unapigia chepuo uhifadhi bora wa baharí na maziwa kama njia mojawapo ya kulinda viumbe vya majini na afya za walaji wa vitoweo.

TAGS:James Waikibia, Kenya, Mazingira, plastiki

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter