Thailand msiwapake matope wanaharakati wa haki za binadamu -UN

17 Mei 2018

Kundi la wataalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ,leo  wamekosoa jinsi utawala nchini Thailand unavyotumia sheria za kuwachafulia majina, kuwapaka matote au kuwaharibia hadhi wanaharakati wa kutetea haki za binadamu  akiwemo  Andy Hall kwa lengo la kumwanyamazisha .

Wanaharakati hao  wamekuwa wakiripoti kuhusu vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu.

Kwa mujibu wa watalaamu hao hilo ni jambo la kushangaza ambapo, kesi za kupakana matope na kuharibiana sifakutumika kama chombo cha kukandamiza haki za kimsingi na za jamii ambapo wenye haki hizo, wakati mwingine, hutoka katika makundi yanayodhurika.

Wameongeza kuwa mashtaka ya makosa ya jinai dhidi ya watetezi wa haki za binadamu nchini hum onia yake nikugandamiza kazi zao na huenda yakakiuka uhuru wa kujieleza.

Bwana Hall amekuwa akikabiliwa na kesi kadhaa  za jinai kwa kufichua madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu tangu Septemba mwaka 2016.

Ufichuaji wake unahusu ukiukwaji wa haki za binadamu kuhusu masuala ya hali za kazi za wafanyakazi  wahamiaji katika kampumi kadhaa za Thailand.

Septemba mwaka 2016 Bwana Hall alikutwa na hatia chini ya sheria za jinai kwa kutimia kompyuta kuchagiza haki  naalihukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha miaka minne pamoja na kupigwa faini ambayo ni sawa na dola za Kimarekani 6,136. Baada ya mwaka mmoja hukumu yake ilibadilishwa na kupunguziwa mwaka mmoja.

Na kisha Machi 26 mwaka 2018, mahakama ya Bangkok ilimuagiza Bw Hall kulipa dola 320,000 kama fidia kwa kampuni moja ambayo ilihusika na moja ya kesi zake.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter