Mwanamke pekee rubani MINUSMA
Huyu ni Sandra Hernandez Vega, raia wa El Salvador ambaye ni rubani wa helikopta ya vita. Anasema ni Imani yake kuwa kupitia kazi yake anachangia mchakato wa amani na utulivu nchini Mali.
Sandra ni mwanamke pekee rubani katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa Mali wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA.
Akiwa na jukumu maalum la kurusha helikopta maeneo mbalimbali kwa lengo la kutoa huduma katika vituo vya walinda amani huko Mali, Bi Hernadez anasema anapenda kazi yake sana na alijifunza kutokana na baba yake mzazi ambaye alikuwa rubani wa ndege..
(Sauti ya Sandra Hernandez Vega )
Nilipokuwa mdogo nilishuhudia sana baba yangu akirusha ndege yake, alikuwa rubani, na kaka zangu wawili ni marubani, mmoja anarusha ndege kubwa na mweingine anarusha elikopta.Nilijivunia sana kuwa nao
Bi Hernadez amejiunga na MINUSMA miaka mitatu iliyopita ambapo kazi yake ni kufanya doria ya usiku na mchana, kutoa msaada wa hali na mali kwa walinda amani nchini Mali.
Sauti ya Sandra Hernandez Vega
Hii ni mara ya kwanza mimi kufanya kazi katika ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa. Kilichonihamasisha kuja hapa ni kwamba ninaweza kuendelea na kazi yangu kama rubani na naweza kutoa huduma kwa raia wa Mali pamoja na nchi yangu. Kwa kurusha elikopta katika doria, ninahisi kuwa ninaweza kusaidia kuleta usalama na utulivu zaidi kwa watu wa Malia. "
Naye Kanali Jose Leon, ambaye ni Mkuu wake amesema anajivunia kuwa na mwanamke kwenye timu yake kwani ni faida kubwa sana linapokuja suala kujenga uaminifu na jamii wanayoihudumia.
Sauti ya Kanali Jose Leon
Kapteni Hernandez Vega ndiye rubani peke wa kike tuliyokuwa naye hapa MINUSMA. Naweza kusema kwamba yeye ni mwanamke shuja , anayestahili kuwa hapa. Alifundishwa pamoja na wanawake wengine. Yeye na marubani wengine wa kiume wako sawa tu . Kuwa naye hapa inatusadia sana kuwa na ukaribu na wakazi wa Mali, akiwa kama mwanamke anakubalika sana hususan pindi anapokuwa karibu na watoto.