Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwendo kasi ndio adui mkubwa wa uhai barabarani

Usalama barabarani.(Picha:UM/21 Centruy/video capture)

Mwendo kasi ndio adui mkubwa wa uhai barabarani

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Zaidi ya watu milioni moja hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, na athari zake sio tu katika familia, bali katika jamii na hata malengo ya maendeleo ya kimataifa. 

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa lengo la kupunguza idadi ya vifo na ajali za barabarani halitoweza kutimia ifikapo mwaka 2030 kama nchi hazitochukua hatua maddhubuti kudhibiti hali hiyo.

Na leo baraza kuu linakuta mjini New york ili kuanzisha kujadili na wakfu maalumu utakaozisaidia nchiwanachama kukabiliana na changamoto na kuboresha usalama barabarani ili kutimiza lengo la maendeleo endelevu SDG la kupunguza ajali hizo kwa asilimia 50.

Wengi wanaopoteza maisha katika ajali za barabarani ni vijana ambao pia ndio nguvu kazi kwa mataifa mengi. Tanzania wadau mbalimbali wameamua kulivalia njuga suala hili kikiwemo chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA kwa nini? Edda Sanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho

(Sauti ya Edda Sanga)

Wanatumia mbinu gani kutimiza azima hiyo?

(Sauti ya Edda Sanga)

Wiki ya Umoja wa Mataifa ya usalama barabarani mwaka huu itafanyika Mei 8-14 kauli mbiu ikiwa kudhibiti mwendo kasi ili kuokoa maisha.