Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali za barabarani ni janga- UN yaanzisha mfumo maalum

Huduma za dharura baada ya ajali kutokea katika moja ya maeneo ya mji wa New  York, nchini Marekani. Huduma za haraka huokoa maisha lakini pia UN inataka hatua madhubuti kuzuia ajali hizo.
UN News/Vibhu Mishra
Huduma za dharura baada ya ajali kutokea katika moja ya maeneo ya mji wa New York, nchini Marekani. Huduma za haraka huokoa maisha lakini pia UN inataka hatua madhubuti kuzuia ajali hizo.

Ajali za barabarani ni janga- UN yaanzisha mfumo maalum

Masuala ya UM

Ajali za barabarani siyo tu zinaleta misiba kwa familia ambazo ndugu au jamaa na marafiki wamepoteza maisha bali pia zinasababisha umaskini kwa sababu fedha zinatumika kwa ajili ya matibabu na wakati mwingine mali hupotea na hivyo mhusika kulazimikakuanza upya maisha.

Umoja wa Mataifa leo umezindua mfuko wake wa kufanikisha harakati za usalama barabarani, wakati huu ambapo inaelezwa kuwa kila mwaka watu milioni 1.3 wanafariki dunia kutokana na ajali za barabarani.

Uzinduzi huo umeenda sambamba na kupitishwa kwa azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lakutambua kuwa idadi ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani imesalia kuwa ya juu kupita kiasi na hivyo kutishia kufanikisha lengo la umoja huo la kupunguza kwa asilimia 50 idadi hiyo ifikapo mwaka 2020.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfuko huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amesema ukuaji wa miji unaongezeka, sambamba na idadi ya watu wanaomiliki magari na miundombinu ya usafiri na matokeo yake..

(Sauti ya Amina J. Mohammed)

“Ajali za barabarani ni sababu ya kwanza ya vifo kwa vijana na zinahusika na kusababisha umaskini kwa mamilioni ya watu kila mwaka.”

Kwa hiyo amesema kwa kupitishwa kwa azimio hilo sambamba na kuanzishwa kwa mfuko huo wa kukabiliana na ajali barabarani..

(Sauti ya Amina J. Mohammed)

 

 “Kuna fursa mpya ya kuhakikisha ushirikiano, ufanisi na hatua zinazoratibiwa.  Natoa wito kwa wadau wa usalama barabarani ikiwemo nchi wanachama wachangie katika mfuko huu na waimarishe juhudi zao za kufanikisha malengo yetu kuhusu usalama barabarani.”

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu usalama barabarani, Jean Todt naye akizungumzia mwelekeo na hatua za kuchukua kudhibiti ajali za barabarani amesema..

Sauti ya Jean Todt)

“Ajali za barabarani zakadiriwa kusababisha hasara ya dola triolioni 1.85 kila mwaka katika uchumi wa dunia na hivyo kudororesha maendeleo endelevu. Kwa hiyo mfuko wa usalama barabarani wa Umoja wa Mataifa hatimaye utaimarisha ushirikiano na uratibu wa uwekezaji kwenye shughuli zinazohusiana na usalama barabarani.”