Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chad taifa la kwanza Afrika kujiunga na mkataba wa maji:UNICE

Maji ni moja ya mahitaji ya msingi ya kuendeleza maisha, lakini kwa wastani watu milioni 117 hawana maji safi na salama katika nchi zinazokumbwa na mgogoro. Picha: UNICEF

Chad taifa la kwanza Afrika kujiunga na mkataba wa maji:UNICE

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Chad imekuwa taifa la kwanza barani Afrika nje ya kanda ya Ulaya kuridhia mkataba wa ulinzi na matumizi ya mipango ya rasilimali ya maji na maziwa ya kimataifa unaosimamiwa na tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Ulaya (UNECE).

UNECE inasema taifa hilo la Afrika ya Kati lisilo na baharí linakabiliwa na changamoto ya udhibiti wa maji na kwa asilimia kubwa linategemea  rasilimali ya maji ilinayoshirikiana na nchi jirani zake za Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Libya, Niger, Nigeria na Sudan.

Katika wakati huu ambao rasilimali ya maji inaendelea kuwa adimu, UNECE inasema kuhakikisha ushirika mzuri baina ya nchi katika udhibiti na matumizi ya maji ni msingi muhimu sana kwa ajili ya maendeleo endelevu , amani na utulivu katika kanda ya Afrika. Jean Rodriguez ni afisa wa UNECE kuhusu mkataba wa maji

(SAUTI YA JEAN RODRIGUEZ)

Ameongeza kuwa kwa kuridhia mkataba huo Chad imethibitisha dhamira yake ya kuhakikisha udhibiti na matumizi endelevu ya rasilimali za maji za kimataifa kupitia misingi na sheria za kimataifa zilizopo na pia kuonyesha mshikamano kwa mkataba huo ambao sasa unapata umaarufu mkubwa duniani kote na hususani barani Afrika.