Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi Kyaka II, Uganda walilia huduma za afya

Huduma bora ya afya ya uzazi inawezesha kukabiliana na ujazito usio wa kupangwa.(Picha:UNFPA/Uganda)

Wakimbizi Kyaka II, Uganda walilia huduma za afya

Msaada wa Kibinadamu

Nchini Uganda wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wahisani wametembelea kituo cha hifadhi ya wakimbizi cha Kyaka II ili kutathmini mahitaji ya kituo hicho na wenyeji wanaokizunguka.

Kituo hicho ambacho sasa kinapokea wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kipo kilometa 200 kutoka mji mkuu Kampala.

Akiwa ziarani hapo Mwakilishi wa UNHCR nchin Uganda, Bornwell Kantande amezungumza na wakimbizi kufahamu mahitaji yao ambapo mmoja wao Gracia Shante amelalamikia ukosefu wa huduma  za afya akisema hakuna dawa na hivyo kulazimu kusaka huduma kwingineko kwa ajili ya watoto wao.

Kwisanga Mizerreo, ambaye ni kiongozi wa ustawi wa wakimbizi ametaka msaada wa fursa za kujiajiri akisema miongono mwao kuna fundi vyerehani, maseremala, vinyozi na hata waendesha bodaboda.

Akijibu hoja hizo Bwana Kantande amesem mpango wa kina wa usaidizi kwa wakimbizi, CRRF unalenga kutoa usaidizi wa aina hiyo na hivyo Uganda inahitaji usaidizi wa kisiasa na kifedha kutoka jamii ya kimataifa ili iweze kuendeleza ukarimu wake kwa wakimbizi.

Amesema ili kufanikisha maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii ni muhimu kushughulikia mahitaji ya wakimbizi na wenyeji wanaowasaidia.

Mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kwenye ziara hiyo ya siku mbili ni pamoja na lile la mpango wa chakula, WFP pamoja na Benki ya Dunia na wawakilishi kutoka Ubelgiji, Ujerumani, Japan, Uholanzi na Sweden.