Ajali ya ndege Urusi imenihuzunisha sana, poleni wafiwa:Guterres

11 Februari 2018

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za ajali mbaya ya ndege iliyotokea leo karibu na mji mkuu wa Urusi Mosco ambapo abiria wote na wafanyakazi wa ndege waliokuwemo wamearifiwa kupoteza maisha.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa, watu na serikali ya shirikisho ya Urusi.

Kwa mujibu wa duru za habari ndege hiyo ya shirika la ndege la Saratov ilianguka dakika chache tu baada ya kupaa kutoka kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo na kuanguka kwenye mji wa Ramenskoye  karibu na Mosco ikikatili maisha ya watu wote 71 waliokuwemo wakijumuisha abiria 65 na wafanyakazi wa ndege 6.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter