Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha hukumu ya kwanza ya maafisa watatu wa jeshi Nepal

UM wakaribisha hukumu ya kwanza ya maafisa watatu wa jeshi Nepal

Umoja wa mataifa umekaribisha hukumu dhidi ya maafisa watatu wa jeshi la Nepali iliyotolewa Jumapili kwa shutuma za kumuua binti wa miaka 15, Maina Sumuwar yapata miaka 13 iliyopita mnamo Februari 2004.

Mahakama ya wilaya imewapatia kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja askari hao hao Babi Khatri, Amit Pun and Sunil Prasad Adhikari kwa mauaji .

Afisa wa nne aliyerejeshwa na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Chad kutokana na hati ya kukamatwa , amefutiwa mashitaka. Hii ni mara ya kwanza wanajeshi wa serikali Nepal kuhukumiwa katika mahakama ya kiraia kwa uhalifu uliotekelezwa wakati wa vita vya 1996-2006.