Ecuador yakosolewa kwa kukandamiza haki

3 Januari 2017

Wataalam maalum wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu wameikosoa serikali ya Ecuador kwa jinsi inakandamiza haki za kiraia kufuatia kitendo chake cha kuamuru kufungwa kwa shirika la kiraia linalotetea haki za watu wa asili na mazingira.

Kwenye taarifa yao waliyotoa huko Geneva, Uswisi, wataalamu hao wamesema mnamo Desemba 18 mwaka jana shirika hilo la 'Acción Ecologica liliomba kwa Tume ya amani na ukweli kuchunguza ukiukwaji wa haki za watu wa asili na zile za mazingira.

Hata hivyo siku mbili baadye Wizara ya Mazingira Ecuador ikaanzisha mchakato wa kulifunga na kulipatia saa 24 za kujibu na siku kumi kuwasilisha utetezi.

Taarifa hiyo imesema kuwa hoja dhidi ya shirika hilo imeanzishwa wakati  mgogoro ambapo watu wa jamii ya Shuar wanapinga uchimbaji madini kwenye eneo wanalodai ni lao.

Kwa mantiki hiyo wataalamu hao wametoa wito kwa mamlaka ya Ecuador kubadili uamuzi wake na kurekebisha sheria inayotumika kufuta shirika hilo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter