Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujitoa EU hakubadili lolote kwa Uingereza:UNHCR

Kujitoa EU hakubadili lolote kwa Uingereza:UNHCR

Uamuzi wa Uingereza kujitoa kwenye Muungano wa Ulaya hakubadilishi lolote , hususani kwa jinsi inavyopaswa kushughulikia waomba hifadhi, limesema Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Ijumaa. Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Taaria ya Flora)

Adrian Edwards msemaji wa Shirika hilo ametoa tangazo hilo kufuatia kura ya maoni ya Alhamisi iliyofanyika England, Wales, Scotland na Ireland Kasakazini, zinazounda Uingereza, ambapo zaidi ya asilimia 52 ya Waingereza wamepiga kura kuunga mkono kujitoa.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)

Hakuna mabadiliko, mkataba wa wakimbizi wa mwaka 1951 bado unatumika. Matokeo ya kura hii ya maoni hayana sauti katika hilo kwa sasa. Mkataba wa kimataifa wa wakimbizi, wajibu wake, wajibu wa Uingereza katika makataba huo, kitaifa katika sheria zake na katika sheria za kimataifa haukuwa sehemu ya kura hiyo ya maoni”

Wakati huohuo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, limesema linaheshimu haki ya uhuru ya Uingereza, lakini linaikumbusha Uingereza kuhusu haja ya kushughulikia uhamiaji kwa usalama, kisheria na njia bora zaidi.