Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ESCAP yaainisha kipaumbele cha Asia-Pacific kabla ya mkutano wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo

ESCAP yaainisha kipaumbele cha Asia-Pacific kabla ya mkutano wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo

Wakati jumuiya ya kimataifa imeanza utekelezaji wa ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu yaani (SDG’s) ukanda wa Asia-Pacific utakuwa na jukumu muhimu, si tu kwa sababu ya ukubwa wa eneo lake, bali tofauti na mabadiliko .

Hayo yamesemwa leo mjini New York na mkuu wa kamisheni ya Umoja wa mataifa ya uchumi na jamii kwa eneo la Asia-Pacific ESCAP katika kuelekea kongamano la baraza la kiuchumi na kijamii ECOSOC la ufadhili kwa ajili ya maendeleo litakaloaanza wiki ijayo.

Dr. Shamshad Akhtar, katibu Mkuu mtendaji wa ESCAP akihutubia wawakilishi wa kudumu wa nchi wanachama wa Umoja wa mataifa amesema katika kuanza mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa ajenda ya mwaka 2030 ESCAP imejikita katika kutanabahi ni jinsi gani ukanda huo umejiandaa na utekelezaji kwa kutathimini mikakati ya utekelezaji wa maendeleo endelevu na pia jinsi gani unaweza kukumbatia na kukusanya rasilimali ili kuzisaidia nchi wanachama katika kufikia malengo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira kupitia mikakati na sera za kitaifa za maendeleo.