Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon afurahia uchaguzi kufanyika kwa amani Burkina Faso

Ban Ki-moon afurahia uchaguzi kufanyika kwa amani Burkina Faso

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefuraishwa na uchaguzi wa wabunge na rais uliofanyika kwa amani nchini Burkina Faso siku ya jumapili hii.

Kwenye taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Bwana Ban amepongeza raia wa Burkina Faso kwa kushiriki kwa wengi uchaguzi huo, hasa wanawake, akisema ushirikiano wao umekuwa dalili ya mshikamano wao kwa utaratibu wa demokrasia.

Wakati ambapo Burkina Faso ikisubiri matokeo ya uchaguzi, Katibu Mkuu amewasihi viongozi wa kisiasa na wadau wengine kukuza hali ya amani nchini humo iliyoenea nchini humo siku ya uchaguzi. Aidha ameziomba pande zote kuendelea kutatua sintofahamu zao kuhusu uchaguzi kupitia njia halali.

Uchaguzi wa tarehe 29 Novemba nchini Burkina Faso umefanyika baada ya mapinduzi ya Oktoba mwaka 2014 na majaribio ya mapinduzi ya mwezi Septemba mwaka huu.