Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kisukari duniani, Ban Ki-moon asisitiza jitihada kwenye nchi zinazoendelea

Siku ya kisukari duniani, Ban Ki-moon asisitiza jitihada kwenye nchi zinazoendelea

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya ugonjwa wa kisukari, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba ugonjwa huo unazidi kuathiri watu wengi duniani hasa kwenye nchi zenye kipato cha chini na cha kati, huku watu wapatao milioni 350 wakiwa wameathirika na ugonjwa huo.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake, Bwana Ban amesisitiza umuhimu wa kupunguza hatari za kuugua ugonjwa wa kisukari, na kusaidia wagonjwa kuishi maisha marefu zaidi.

Taarifa imeeleza pia kwamba wagonjwa wa kisukari wanaweza kupata mshtuko wa moyo, upofu, kushindwa kwa figo au kukatwa kwa viungo vya chini.

Katibu Mkuu ameongeza kwamba hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuepusha ugonjwa wa kisukari aina ya 2, ule unaowakumba watu wanene, ni zile zile za kuishi maisha yenye afya bora, ikiwa ni pamoja na kutembea kila siku na kufanya mazoezi.

Aidha Bwana Ban ameeleza kwamba matibabu ya ugonjwa wa kisukari ni ghali na hivyo gharama hizo hukumba watu wengi na hivyo akaziomba serikali kuimarisha huduma za afya kwa wagonjwa wa kisukari na kurahisisha upatikanaji wa matibabu.