Skip to main content

Tusisahau ukanda wa maziwa makuu: mwanadiplomasia wa Ufaransa

Tusisahau ukanda wa maziwa makuu: mwanadiplomasia wa Ufaransa

Bado matatizo ni mengi na mawingu yameongezeka katika ukanda wa maziwa makuu, ameeleza Jean Christophe Belliard, mkuu wa idara ya ukanda wa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa.

Amesema hayo akishiriki mkutano wa sita wa kikanda kuhusu mchakato wa amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na ukanda wa maziwa makuu, uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na viongozi wa ukanda huo.

Akihojiwa na Priscilla Lecomte wa idhaa hii, ameanza kwa kueleza mtazamo wake kuhusu hali ilivyo kwenye ukanda huo.