Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa watekeleza miradi ya maendeleo Tanzania

Umoja wa Mataifa watekeleza miradi ya maendeleo Tanzania

Kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa na ukomo wa mipango ya maendeleo ya milenia MDGs Umoja huo katika nchi mbalimbali umekuwa ukifanya miradi ya maendeleo inayolenga kuinua vipatao vya nchi husika.

Nchini Tanzania UM umeanzisha miradi kadhaa ikiwamo ya elimu, kilimo ,uvuvi na mengineyo. Kufahamu namna miradi hii ilivyotekelezwa na kubadilisha maisha ya watu ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo