Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu milioni 13 wameathirika na kimbunga Haiyan:OCHA

Watu milioni 13 wameathirika na kimbunga Haiyan:OCHA

Idara ya ustawi wa jamii na maendeleo ya Ufilipino inakadiria kwamba watu milioni 13 wameathirika na kimbunga Haiyan na wengine milioni 4 wametawanywa , limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA.

OCHA imeongeza kwamba watu zaidi ya 392,000 wanaishi katika vituo vya muda 1,587 ambavyo vingi vipo majimbo ya Magharibi na Mashariki ya Visayas. Karibu nyumba milioni 1.1 zimeathirika na kimbunga hicho na takribani nusu yake zimebomolewa kabisa.

OCHA inasema ufadhili wa misaada ya kibinadamu hadi sasa ni dola milioni $195 na dola mmilioni 87 kati ya hizo zimechangiwa na Umoja wa Mataifa  na washirika wao wana mpango wa kutoa dola milioni 301.