IAEA yakamilisha uchunguzi Australia

15 Novemba 2013

Timu ya wataalamu wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu nguvu za atomiki IAEA leo limekamilisha tathimini ya usalama nchini Australia namna taifa hilo linavyochukua hatua za usalama kuhusiana na matumizi ya nukilia.

Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa wamekuwa nchini humo kwa muda wa wiki mbili ambako pa moja na kufanya ukaguzi wa mitambo lakini pia walipitia ripoti mbalimbali zilitolewa na serikali ya Australia.

 Ziara ya wataalamu hao nchini Australia ni sehemu ya nchi sita ambazo wataalamu hao wamezitembelea na kuendesha uchunguzi.

Mkuu wa ujumbe huo Kristóf Horváth amesema kuwa ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa hasa kutokana na kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa maafisa wa serikali, mashirika ya kiraia pamoja na wataalamu wa mionzi.