Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya haijajitoa ICC: Waziri Amina Mohammed

Kenya haijajitoa ICC: Waziri Amina Mohammed

Waziri wa masuala ya kigeni wa Kenya amehitimisha ziara yake ya kikazi mjini New York na kuzungumzia kura iliyopigwa na bunge la Kenya ya kutaka nchi hiyo kujiondoa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Serikali ya Kenya haijajitoa ICC lakini kile kilichofanyika ni Bunge kutekeleza haki yake ya msingi ya kupigia kura hoja wanayotaka itekelezwe kwa mujibu wa matakwa ya wananchi. Ni kauli ya Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohamed aliyotoa katika mahojiano maalum na Idhaa hii akizungumzia suala la bunge la Kenya kupiga kura ili Kenya ijiondoe ICC kufuatia mashataka dhidi ya viongozi wa nchi hiyo akiwemo Rais Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto.

(SAUTI YA AMINA)

Kuhusu athari ya Kenya kujiondoa ICC siku za usoni Waziri Mohamed amesema, Kenya ilitia saini mkataba wa Roma na mkataba huo huo unasema kwamba nchi inaweza kujiondoa, akiongeza kuwa halitakuwa tukio la kwanza kuwahi kufanyika lakini kwa sasa bado halijafanyika kwa sababu

(SAUTI YA AMINA)

Waziri Mohamed amezungumza hayo dakika chache baada ya kuhudhuria kumbukumbu iliyofanyika Jumatano hapa New York kwa ajili ya watu waliopoteza maisha kwenye shambulizi la kigaidi huko Westgate, Nairobi Kenya, Tukio hilo lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 60 huku wengine zaidi ya 150 wakijeruhiwa.