Malawi na WFP wazindua operesheni kukidhi mahitaji ya chakula:

2 Oktoba 2013

Serikali ya Malawi pamoja na shirika la mpango wa chakula duniani na wadau wengine wamezindua operesheni ya misaada ili kukidhi mahitaji ya chakula yanayoongezeka kutokana na hali mbaya ya hewa msimu wa kupanda na kupanda kwa bei Alice kariuki na taarifa kamili:

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Kwa mujibu wa serikali ya Malawi maenmdeo yanayohitaji chakula yameongezeka ikilinganishwa na mwakajana na yanajumuisha pia sehemu ambazo kwa kawaida huwa kama maghala ya kuhifadhi chakula ya mikoa ya Kati na Kaskazini mwa Malawi.

Zaidi ya watu milioni 1.46 watahitaji msaada wa chakula nchini humo katika miezi ijayo imesema kamati ya taifa ya tathimini kwa mwezi wa Julai MVAC. Inaaminika kwamba idadi hiyo itaongezeka na WFP inajiandaa kuongeza operesheni zake za msaada kwenda sambamba na mahitaji .

Msimu wa mavuno uliopita watu milioni 1.9 walihitaji msaada wa chakula katika wilaya 16, msimu huu wilaya 21 kati ya 28 zitaathirika na njaa kwa mujibu wa tathimini ya Julai ya MVAC inayojumuisha wadau kutoka Malawi, mashirika ya Umoja wa mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali.