Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukanda wa Sahel wazidi kumulikwa, Maurtania yataka jumuiya ya kimataifa kunusuru uhalifu.

Ukanda wa Sahel wazidi kumulikwa, Maurtania yataka jumuiya ya kimataifa kunusuru uhalifu.

Waziri wa mambo ya nje wa Mauritania Ahmed Ould Sid' Ahmed ni miongoni mwa viongozi waliohutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa katika mjadala wa mwisho wa juma ambapo pamoja na kugusia utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia nchini mwake ameungana na viongozi wengine wa Afrika kulaani matukio ya ugaidi hususani lile la hivi karibuni nchini Kenya huku pia akiitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia ukanda wa Sahel katika kupambana na changamoto mbalimbali za kihalifu.

 (Sauti ya Ahmed)

Ukanda wa Sahel kwa muda mrefu umekabiliwa na uhalifu wa kupangwa kwa namna mbalimbali kama vile madawa ya kulevya, usafirishaji  haramu ya silaha , usafirishaji haramu wa binadamu, uhamijai haramu na utekaji wa mateka, natoa wito kwa jumuiaya ya kimataifa kusaidia ukanda huu  ili kukabiliana na hatari hizi

 Kuhusu kuimarisha demokrasia nchini mwake amesema uchaguzi ujao utakaotoa fursa kwa wananchi kushiriki kikamilifu  ni kielelezo cha mustakabali mwema wa demokrasia nchiniMauritania.