Misaada ya kibinadamu yaangaziwa nchini Tanzania
Wiki hii dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usaidizi wa Kibinadamu ambapo Umoja wa Mataifa umefanya kumbukumbu ya watumishi wake waliopoteza maisha wakiokoa maisha ya wengine. Kauli mbiu mwaka huu ni Dunia inahitaji misaada zaidi.
Kwa kutambua uzito huu, katika makala yetu leo mwenzetu George Njogopa anamulika hali ya misaada ya kibinadamu nchini Tanzania ambako pia inaendelea kuhifadhi wakimbizi kadhaa wa Burundi walioko katika kambi ya Nyarugusu iliyoko Mkoani Kigoma. Karibu kuungana naye: