Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha kurithiwa sheria ya utaratibu wa uchaguzi Afghanistan

Ban akaribisha kurithiwa sheria ya utaratibu wa uchaguzi Afghanistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha hatua ya rais wa Afghanistan kurithia sheria inayodhibiti mifumo na wajibu wa taasisi za kusimamia uchaguzi nchini humo.Bwana Ban amesema sheria hiyo ni hatua muhimu katika kuweka utaratibu thabiti wa uchaguzi wa urais na mabaraza ya mikoa, ambao utafanyika mnamo April 5 mwakani.

Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban anatarajia sheria hiyo itekelezwe haraka ili kuwezesha uchaguzi ulo wazi, wa kuaminika na jumuishi.

Amekaribisha pia kuidhinishwa kwa sheria kuhusu uchaguzi wiki hii na bunge la nchi hiyo, ambayo inabainisha utaratibu wa kisheria kwa harakati zote za uchaguzi nchini Afghanistan.