Watakiwa kuhama kuepuka madhara ya kimbunga nchini Myanmar

16 Mei 2013

Wakati watu na serikali ya Myanmar wakikabiliwa na kimbunga Mahasen Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini humo Bwana Ashok Nigam ametaka kuhamishwa haraka kwa watu watakaoathirika.Mapema, serikali ya Rakhine imeripoti kwamba zaidi ya watu 35,000 wamehamishwa pamoja na watu wanaioshi makambini. Maelfu ya watu katika eneo hilo walilazimika kuhama makazi yao wakati wa ghasia mwaka 2012 ambapo Rakhine ni eneo linalotarajiwa kuathiriwa kwa asilimia kubwa na kimbunga hicho mwishoni mwa wiki hii.

Kirsten Mildren ni Afisa mawasiliano na utetezi wa ofisi ya kanda ya kuratibu misaada ya kibinadamu katika Asia Pacific

(SAUTI YA KRISTERN MILDRED)

"Hakika kumekuwa na maandalizi ya kutosha nchini Myanmar tumekuwana wiki nzima ya kujiandaa ambayo imefanyika vyema na hata sasa mashirika ya muoja wa mataifa na taasisi nyingine bado wanaendelea na operesheni, misaada imekuwa ikiwekwa tayari na kesho wataendesha tathimini kutambua kiwango cha uharibifu na kuanza haraka kugawa misaada. "