Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa Malaria bado ni tatizo nchini Burundi

Ugonjwa wa Malaria bado ni tatizo nchini Burundi

Wakati siku ya Malaria duniani ikiangaziwa tarehe 25 Aprili na ujumbe Wekeza kwa baadaye tokomeza Malia, nchini Burundi takwimu zinayonesha kuwa asilimia 21 ya wananchi husumbuliwa na maradhi hayo. Ugonjwa huo umekuwa tatizo la kwanza la afya. Wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano ndio wanaathiriwa sana na Malaria.

Lakini takwimu za mwaka wa 2012 zinaonyesha kuwa maradhi ya Malaria yamepunguwa kwa asilimia 20 hasa kutokana na matumizi ya vyandarua vyenye dawa. Rioti hii fupi ya mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani Kibuga inafafanua zaidi.