Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mashambulizi ya bomu Boston

Ban alaani mashambulizi ya bomu Boston

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani vikali mashambulizi ya bomu yalotekelezwa leo siku ya Jumanne mjini Boston, Marekani wakati wa mashindano ya kimataifa ya mbio za masafa marefu, maarufu kama Boston Marathon.

Mashambulizi hayo yameripotiwa kuwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine kadhaa. Akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda miaka 19 iliyopita, Bwana Ban amesema, wakati maelezo zaidi yakisubiriwa, anawapa pole wote walowapoteza jamaa zao na wale walojeruhiwa katika mashambulizi hayo.

(SAUTI YA BAN)