Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu mkuu amteua Stephen Cutts wa Uingereza mahala pa Warren Sachs

Katibu mkuu amteua Stephen Cutts wa Uingereza mahala pa Warren Sachs

Katibu Mkuuu wa UM Ban Ki-moon amemteua Stephen Cutts wa Uingereza kama msaidizi ofisi kuu ya huduma kwenye idara ya menejimenti.

Anachukua nafasi ya Warren Sachs ambaye Katibu Mkuu amemshukuru kwa kujitoa kwa dhati katika majukumu yake.

Bw. Cutts ana uzoefu mpana wa Mashirika ya Kimataifa na ana uwezo wa kusimamia mabadiliko yatakayochangia kuimarisha ufanisi.

Bw. Cutts ameshika nafasi za juu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Commonwealth ikiwemo usimamizi wa fedha na utekelezaji, kupanga mikakati na rasliamali  watu.