Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali inazidi kuzorota Syria: UNHCR

Hali inazidi kuzorota Syria: UNHCR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema hali inaendelea kuzorota nchini Syria ikiwemo katika maeneo ya Kati na viunga vya Damascus na hivyo kusababisha ongezeko la wakimbizi.

Shirika hilo linasema sasa kuna hofu ya usalama wa kikanda wakati idadi ya wakimbizi waliohama nhi hiyo nakwenda Misri, Iraq, Jordan, Lebanon na Uturuki ikifikia zaidi ya milioni 1.2.

UNHCR inasema tangu Januari mosi mwaka huu imesajili wakimbizi 477,347. Mipango ya kikanda kukabiliana na hali ya wakimbizi inaendelea na fedha zilizopatikana ni asilimia 31 tuu ya dola milioni 735 zinazohitajika.