Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi wa habari wa radio nchini Brazil

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi wa habari wa radio nchini Brazil

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO Irina Bokova amelaani mauaji ya mwandishi wa habari wa Brazil  Mafaldo Bezzera Goes aliyeuwawa kwa kipigwa risasi. 

Bibi Bokova katikaa tamko hilo la kulani mauaji ya mwandishi Mafaldo,ametaka uchunguzi wa kina juu ya mauaji hayo ufanyike na wauaji wafikishwe katika vyombo vya sheria.

Pia amesema mauaji kama hayo ni laziam yakomeshwe kwa kuwa yanaingilia uhuru wa vyombo vya habari na kuhatarisah maisha ya wanahabari.