Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran iache kukamata waandishi wa habari: Wataalamu UM

Iran iache kukamata waandishi wa habari: Wataalamu UM

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya haki za binadamu wametoa wito kwa serikali ya Iran kusitisha hatua yake ya kuwakamata waandishi wa habari na kuwaachilia wale ambao bado wanazuiliwa.

Wito huo unajiri baada ya tukio la juma lililopita ambapo maafisa wa usalama walivamia afisi za magazeti matano na kuwakamata takriban waaandishi wa habari 17 wengi wakiwa ni wale wanaojitegemea.

Wataalamu hao wanasema kuwa hatua hiyo ya hivi majuzi ya kuwakamata waandishi wa habari wakiwa wanatekeleza majukumu yao ni sehemu ya kampeni ya kuwakandamiza waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini Iran, na inakiuka wa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.