CERF yatoa fedha na kupambana na njaa nchini Malawi

15 Januari 2013

Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umeidhinisha kutolewa kwa dola milioni 3.2 zitakazotumiwa kupambana na tatizo la ukosefu wa chakula nchini Malawi nchi ambayo zaidi ya nusu ya wananchi wake wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku huku asilimia 46 ya watoto walio chini ya miaka wakiwa na matatizo ya kukua.

Kutokana na misimu ya kiangazi iliyoshuhudiwa inakadiriwa kuwa takriban watu miilioni 1.97 ambayo ni asilimia 13 ya watu wote nchini Malawi wanaorodhewa kuwa wasio na usalama wa chakula. Kutokana na hilo CERF ilitoa fedha ambazo zitagharamia huduma za kuokoa maisha kwa wanaoathiriwa na ukosefu wa chakula. CERF ilitoa jumla ya dola milioni 1.8 kwa Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF kufadhili huduma kwa watoto wanaosumbuliwa na utapiamlo.