Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kujielisha kuhusu usalama wa nukilia wakamilika Japan

Mkutano wa kujielisha kuhusu usalama wa nukilia wakamilika Japan

Naibu mkurugenzi mkuu kwenye masuala ya usalama wa nuklia kwenye Shirika la kudhibiti nishati ya atomic duniani IAEA Denis Floy amesema kuwa mkutano ambao umekamilika umetoa fursa nzuri wa kubadilishana ujuzi kutokana na ajali ya kituo cha Fukushima Daichi nchini Japan na pia kutoa mwelekeo wa kuwepo jitihada za kimataifa za kuhakikisha kuwepo usalama wa nishati ya nuklia.

Amesema kuwa mkutano huo umekuwa ni wakati mzuri kwa nchi kuahidi kutekeleza usalama kwa nishati ya nuklia na kufahamu hali waliyopitia wafanyikazi walipokuwa wakikabiliana na ajali iliyotokea. Kwa upande wake naibu mkurugenzi kwenye tume inayohusika na nishati ya nuklia nchini Canada anasema kuwa inahitajika kuwe na ushirikiano kutoka kwa IAEA, kutoka kwa wanachama na washikadau. Nchi 117 pamoja na mashirika 13 ya kimataifa walihudhuria mkutano huo uliokuwa na lengo la kuelisha kutokana na ajali ya kituo cha nuklia cha Fukushima Daichi na kujadili njia za kuhakikisha kuwepo usalama wa nishati ya nuklia.