Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya kimbunga Bopha Ufilipino, maisha ya watoto yako hatarini

Baada ya kimbunga Bopha Ufilipino, maisha ya watoto yako hatarini

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema kuwa watoto waliobakia bila makazi katika maeneo yaliyokumbwa na kimbunga huko Ufilipino wako hatarini kunyanyaswa na kutumikishwa.

UNICEF inasema licha ya kwamba kazi nzuri imefanyika kukabiliana na madhara ya kimbunga, lakini mahitaji muhimu ya watoto hayatiliwi maanani na hivyo kuwaweka hatarini zaidi kudhalilika ikiwemo kusafirishwa kinyume cha sheria. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)