Dola milioni 65 zahitajika kusaidia Ufilipino baada ya Kimbunga Bopha

10 Disemba 2012

Umoja wa Mataifa na washirika wake wa kibinadamu leo wametoa ombi la dola milioni 65 kutoka kwa jumuiya ya kimataifa ili kusaidia mamilioni ya watu walioathirika kutokana na Kimbunga Bopha huko Ufilipino.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), fedha zitatumika katika Mpango unaojulikana kama Action Recovery Plan unavyoeleza jinsi mashirika ya kibinadamu yakiwemo yale ya Umoja wa Mataifa , yasiyo ya kiserikali yakishirikiana na serikali yatatoa msaada kwa muda wa miezi sita ili kukidhi mahitaji muhimu ya waathirika hao.

Mratibu wa OCHA nchini Ufilipino Luiza Carvalho, amesema ameshuhudia vijiji na nyumba zikiwa zimesambaratishwa hali iliosababisha watoto na wanawake ikiwemo wajawazito kubaki bila makazi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter