Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaanzisha mpango wa kuwanufaisha wasomali na bidhaa za mifugo

FAO yaanzisha mpango wa kuwanufaisha wasomali na bidhaa za mifugo

Shirika la kilimo na mazao la Umoja FAO limeanzisha mpango ambao utawawezesha wenyeji wa taifa la Somalia kunufaika na bidhaa za mifugo kama vile ngozi na mifupa ya ngamia. Baada ya miongo miwili ya vita na ukame, Somalia haijakuwa na viwanda vya nyumbani vinavyoweza kutengeza bidhaa kama vile sabuni.

Katika eneo la Somaliland ambalo hakijaathiriwa sana na mapigano kuna matumaini na mfano ambao utafautwa na nchi nzima. Somalia ni taifa ambalo mifugo uuzwa kwa kimo na kwa uzani lakini sasa kupitia programu hii wengi wameweza kugundua thamani iliyo kwa mifugo hawa awe mbuzi au ngamia. Kutoka na kukamilika kwa progamu ya kwanza mwezi Julai mwaka 2012 awamu ya pili ya mpango huu sasa ina mipango ya kubuni nafasi zaidi za ajira kote nchini Somalia.