Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya amani na kibinadamu Ukanda wa Gaza ni mbaya: UNRWA

Hali ya amani na kibinadamu Ukanda wa Gaza ni mbaya: UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada na ulinzi kwa wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limesema hali ya usalama na kibinadamu huko Ukanda wa Gaza ni mbaya.

Msemaji wa UNRWA Christopher Gunnes akizungumza na radio ya Umoja wa Mataifa hii leo amesema wanachoshuhudia hivi sasa ni maroketi yakirushwa kwenye eneo hilo la Gaza ambalo nusu ya wakazi Milioni Moja nukta saba wa eneo hilo ni watoto.

Amesema idadi ya vifo vinaongezeka na kwamba huduma za afya katika hospitali kuu huko Gaza imezidiwa uwezo hivyo pande husika hazina budi kusitisha mapigano .

Tunachoona hivi sasa ni maroketi yanarushwa kutoka eneo hili ambalo nimesema lina idadi kubwa ya watu na wengi wao ni raia. wakazi wake wengi ni raia na mashambulio ya anga yanatua hapa. Kwa hiyo hali ni mbaya na ndio maana sisi hapa UNRWA tnaunga mkono kauli ya Katib Mkuu Ban Ki-Moon ya kusihi pande zote kujizuia na kuacha mkondo wa amani uanze kuchukua nafasi yake.pande zote zinapaswa kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kulinda raia, idadi ya vifo vya raia inaongezeka na itazidi kuongezeka iwapo wito wa Bwana Ban hautasikilizwa na pande husika.”