Cambodia yatuhumiwa kubinya vyama vya kiraia

16 Novemba 2012

Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema mwelekeo uliochukuliwa na utawala wa Cambodia katika wakati mataifa ya eneo la Asia na Pacific yakijiandaa na mkutano wa kilele wa ASEAN unatia shaka.

Duru kutoka Cambodia zinasema kuwa maafisa wa serikali wamekuwa wakifuatilia kwa karibu utendaji kazi pamoja na shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali katika kile kinachoelezwa kukusanya taarifa za udokozi.

Utawala huo wa Cambodia pia unaarifiwa kukusanya taarifa za mashirika ya kiraia kutoka nchi wa eneo zitakazohudhuria mkutano huo uliopangwa kufanyika mwishoni mwa juma.

Kiasi cha watu wasiopungua 60 wanasemekana wamekamatwa na maafisa wa serikali kama sehemu ya kubinya mijadala inayoangazia haki za binadamu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud