Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa dawa za kuzuia kichocho nchini Nigeria

WHO yatoa dawa za kuzuia kichocho nchini Nigeria

Shirika la Afya Duniani, WHO, limetoa zaidi ya tembe milioni tano za kuuwa minyoo inayosababisha ugonjwa wa kichocho kwa serikali ya Nigeria, ili kusaidia kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo unaoainishwa miongoni mwa magonjwa ya kitropikali yalosahaulika.

Idadi ya watu watakaolindwa kutokana na ugonjwa huo inakadiriwa kuwa milioni tatu.

Ugonjwa wa kichocho huzuia ukuaji wa mwili na viungo kama akili, na kusababisha kukosa damu miongoni mwa watoto na akina mama waja wazito, na kuongeza hatari ya kuzaa watoto wenye uzani wa chini. Alice Kariuki na taarifa kamili