Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la waasi, Serikali ya Sudan zakubaliana kurejea kwenye meza ya mazungumzo

Kundi la waasi, Serikali ya Sudan zakubaliana kurejea kwenye meza ya mazungumzo

Maafisa wa serikali ya Sudan na wale wa kundi la waasi wamekubaliana kwa msingi kuendelea na duru la majadiliano na tayari pande zote mbili zimetiliana saini itifaki inayotambulisha utayari wa kukaribisha meza ya majadiliano.

Kundi la Usawa na Haki ambalo ni miongoni mwa makundi ya waasi katika eneo la Darfur lilichangia kuzorotesha usalama wa eneo hilo limekubali kuweka chini silaha na kuanzisha duru ya majadiliano ya amani.

Makubaliano hayo ya kuendelea na majadiliano ni utekelezaji wa vipengele muhimu vilivyofikiwa kwenye majadiliano ya amani ya Doha ambayo yanahimiza kukomeshwa machafuko na kupisha dura ya majadiliano.

Pande hizo mbili zimekubaliana kuanza kukutana kwa majadiliano ya amani mara baada ya kupita sikukuu ya Eid Al-Adha inayotazamiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu wa kumi.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na ujumbe wa vikosi vya kimataifa vinavyolinda amani Darfur UNAMID majadiliano hayo yatafanyika Qatar, Doha ambako ndiko pahala kulikoanzishwa majadiliano ya usakaji wa amani