Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR yashtushwa na wimbi la mauwaji Guatemala

OHCHR yashtushwa na wimbi la mauwaji Guatemala

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayojihusisha na haki za binadamu imeelezea kushishtushwa kwake kutokana na ongezeko la mauwaji ya watu nchini Guetemala na tukio la hivi karibuni la kuuliwa kwa wakulima.

Ripoti zinasema kuwa vurugu zilizotokea hapo alhamisi baina ya wakulima wazawa na makundi ya polisi na askari katika eneo la Magharibi mwa Guetamala, imesababisha wakulima 6 kuuwawa na wengine 30 wakijeruhiwa.

Katika vurugu hizo zilizotokea katika idara ya Totonicapan askari wapatao 7 walijeruhiwa pia.

Duru za vyombo vya habari zinasema kuwa chanzo cha vurugu hizo zilitokana na wakulima kwenye eneo hilo kuweka vizuizi kwenye bara bara kama njia ya kuwasilisha malalamiko yao kutokana na kuongezeka kwa gharama za umeme kwenye baadhi ya huduma.