Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kunahitajika mashirikiano ya dhati ili kufikia malengo ya milenia:Viongozi wa Afrika

Kunahitajika mashirikiano ya dhati ili kufikia malengo ya milenia:Viongozi wa Afrika

Viongozi wa Afrika wamesema kuwa kuna haja kwa jumuiya ya kimataifa kuanzisha mbinu mpya za kulisaidia bara hilo ili lifaulu kwa wakati kutimiza malengo ya maendeleo ya mellenia.

Maraia kutoka Zambia na Ghana wameimbia hadhara ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuwa afrika inapaswa kusaidia hasa wakati huu ambapo kipindi cha kutimiza malengo ya mellenia kikikaribia.

Rais Michael Sata wa Zambia amesema kuwa wakati nchi yake ikiwa kwenye mkondo sahihi kwa kufaulu kupiga hatua kwenye baadhi ya malengo lakini kwa ujumla wake maeneo mengi ya afrika bado yanasua sua hivyo kuna haja ya kuungwa mkono ili kufaulu kwa wakati.

Kauli kama hiyo imetolewa na rais wa Ghana John Dramani Mahama ambaye amesema kuwa nchi yake haina wasiwasi juu ya ufikiaji wa malengo hayo ya melenia lakini amesisitiza bado kuna hitajika uungwaji mkono katika baadhi ya maeneo.

Nchi hizo mbili zinatajwa kufanya vizuri kwenye maeneo ya afya, elimu lakini zinakabiliwa na mkwamo kwenye maeneo mengine.