Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waanzisha fursa mtandaoni kutoa uzoefu nchi zilizopitia vita

UM waanzisha fursa mtandaoni kutoa uzoefu nchi zilizopitia vita

Umoja wa Mataifa umezindua kile kinachoitwa fursa mtandaoni ambao utatoa nafasi kwa nchi mbalimbali duniani kuwasilisha uzoefu wa baada ya vita.

Mtandao huo unalenga na kuzipa nafasi nchi ambazo zilitumbukia kwenye machafuko ya kivita kuelezea michakato iliyopitia baada ya kuishi kwa kipindi cha uhasama.

Wavuti huo unakusudia kutoa fursa kwa makundi yote ya watu ikiwemo watu binafsi,na taasisi za kiserikali.

Nchi za kwanza kushiriki kwenye fursa hiyo ni pamoja na Indonesia, Afrika Kusin, Morocco, Brazil, Misri na Benin. Nchi nyingine ni Kenya, Thailand na Nigeria.

Pia kunamashirika ya kiraia kutoka Norway, Canada, Ujerumani,Uingereza na Sweden