Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaanza kusambaza chakula kwa waathirika wa mafuriko Pakistan

WFP yaanza kusambaza chakula kwa waathirika wa mafuriko Pakistan

Shirika la Mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP limeanza kusambaza huduma ya chakula kwa mamia ya watu walioathirika na mafuriko katika jimbo la Sindh nchini Pakistan

Shirika hilo limesema linakusudia kuyafikia maeneo yote ambayo yaliathiriwa na mafuriko hayo.Familia nyingi kwenye eneo hilo bado zinaendelea kuishi maisha ya shida na taabu kutokana na makazi yao kuharibiwa na mafuriko hayo.

Pamoja na uharibifu wa nyumba na maisha ya watu, mafuriko hayo yariharibu miundo mbinu na kufanya ustawi wa eneo hilo kuanguka chini.

Katika hatua zake za awali WFP inasambaza huduma za chakula kama unga, mboga za majani pamoja na mafuta kwa wahitaji.