Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha wanajeshi 2,500 zaidi katika vikosi vya kikanda vinavyokabiliana na LRA

UM wakaribisha wanajeshi 2,500 zaidi katika vikosi vya kikanda vinavyokabiliana na LRA

Umoja wa Mataifa umekaribisha kuingizwa kwa wanajeshi 2,500 katika vikosi vya pamoja vya Muungano wa Afrika ambavyo vimewekwa ili kukabiliana na waasi wa LRA. 2, 000 kati ya wanajeshi hao ni kutoka kwa jeshi wa Uganda, na 500, kutoka jeshi la Sudan Kusini.

Waasi wa LRA wanajulikana hasa kwa ukatili ambao walitekeleza nchini Uganda, ingawa katika miaka ya hivi karibuni wamehamia nchi jirani katika kanda ya Afrika Mashariki ambako wanaendelea kutekeleza unyama wao.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo ya kuuingizwa wanajeshi wapya katika vikosi vinavyomsaka Joseph Kony na LRA, mwakilishi maalum ambaye pia ni mkuu wa afisi ya kanda ya Afrika Mashariki ya Umoja wa Mataifa, Abou Moussa amesema hatua hiyo ni matokeo ya juhudi za pamoja za kutokomeza vitendo vya LRA, kundi la waasi ambalo limechangia mateso na uchungu mwingi kwa raia katika nchi zilizoathirika. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)